Taarifa kamili kuhusu madhara ya tetemeko la ardhi Kagera
Moja
ya headline zilizochukua nafasi katika vyombo mbalimbali vya habari na
baadhi ya mitandao ya kijamii ni pamoja na hili la September 10 2016
lilohusisha tetemeko la ardhi katika mkoa wa Kagera na kusababisha vifo vya watu kadhaa huku wengine wakijeruhiwa na hata kupoteza makazi.
Leo
September 13 2016 Serikali imeliongelea tukio hilo bungeni Dodoma ambapo
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa – TAMISEMI George Simbachawene amezungumza kwaniaba ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Simbachawene amesema…>>>’September
10 2016 majira ya saa 9 alasiri mkoa wa Kagera ulipatwa tetemeko la
ardhi lenye ukubwa ambalo limesababisha maafa makubwa kwa wakazi wa
maeneo hayo‘
‘Idadi
ya vifo vilivyoripotiwa katika mkoa huo hadi sasa ni 17, majeruhi 252
ambapo nyumba za makazi zilizoanguka ni 840 na nyumba zenye nyufa ni
1264‘ –Waziri Simbachawene
‘Serikali imeagiza Halmashauri ya Bukoba kufunga kwa muda shule za Ihundo na Nyakato serikali Bukoba kwa kuwa zina hali mbaya‘ –Waziri Simbachawene
‘Serikali
inatoa wito kwa wananchi na Kagera na maeneo yote yalioathirika kuwa
watulivu na kuonyesha ushirikiano ili kuhakikisha changamoto zilizopo
zinatatuliwa kwa kasi ili kupunguza ukubwa wa madhara ya tukio‘-Waziri Simbachawene
Taarifa kamili kuhusu madhara ya tetemeko la ardhi Kagera
Reviewed by pongwa trading
on
22:45:00
Rating:
No comments