Home Top Ad

Responsive Ads Here

Sirro aapishwa rasmi kuwa IGP

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amemvisha cheo kipya na kumuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya (IGP) Simon Sirro Ikulu Jijini Dar es Salaam

Baada ya kuapishwa (IGP) Sirro alikula kiapo cha uadilifu kwa uongozi wa umma na kuahidi kuwa atakuwa mzalendo kwa nchi yake ya Tanzania na mtii wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Nitakuwa muadilifu na mfano wa watumishi wa umma na watu wengine katika kukuza na kusimamia maadili, sitatumia cheo changu na wadhifa wangu kwa maslahi binafsi ya familia yangu, ndugu zangu au marafiki zangu, isipokuwa kwa maslahi ya umma. Nitalinda na kuitumikia rasilimali ya umma kwa maslahi ya umma, nitatekeleza majukumu yangu kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni na taratibu na miongozo kwa maslahi ya umma. Sitaomba wala kushawishi kutoa au kupokea rushwa" alisema Sirro
Sirro aapishwa rasmi kuwa IGP Sirro aapishwa rasmi kuwa IGP Reviewed by Unknown on 02:22:00 Rating: 5

No comments

Recent