Home Top Ad

Responsive Ads Here

INSTAGRAM-Shamsa amuoneaa wivu Odama

Malkia wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameweka wazi kumuonea wivu mahusiano ya muigizaji mwenzake, Jenipher Kyaka 'Odama' kwa kuyafanya kuwa na usiri mkubwa huku akipongeza na kusema ndivyo inavyopaswa mtoto wa kike kufanya kwenye mapenzi.

Shamsa amefunguka hayo na kusema anapenda jinsi muigizaji huyo anavyoweza kuweka mahusiano yake ya mapenzi kuwa faragha yake peke yake na kuongeza kuwa anatamani kama siku zingerudi nyuma asingethubutu kumuonyesha mpenzi wake hadharani bali mume wake wa ndoa.

"Napenda unavyoweka mahusiano yako ya mapenzi 'private'. Sijawahi ona hata siku moja umempost sijui boyfriend na hicho ndo kitu kizuri kwa mtoto wa kike. Mimi kwa upande wangu ningerudisha siku nyuma kipindi kile nipo single nisingempost au kumuweka wazi mwanaume yoyote niliyekuwa naye kipindi kile kwenye mahusiano. Natamani mume wangu ndio angekuwa mwanaume wa kwanza kwa watanzania kumjua" - Shamsa Ford alifunguka.
INSTAGRAM-Shamsa amuoneaa wivu Odama INSTAGRAM-Shamsa amuoneaa wivu Odama Reviewed by Unknown on 03:14:00 Rating: 5

No comments

Recent