Home Top Ad

Responsive Ads Here

Nuh Mziwanda- sihitaji kollabo

Msanii wa bongo fleva anaye 'hit' na ngoma 'Anameremeta' Nuh Mziwanda amefunguka kwa kusema hataki kolabo na wasanii wa nje ya kwa sasa kwa kile anachokiamini muziki wake una ladha nzuri ndani ya nchi.


Nuh amebainisha hayo baada ya wasanii wengi wa sasa wakidhani kufanya kazi na wasanii wa kimataifa ndiyo njia itakayowapelekea kupata mafanikio zaidi katika kazi zao.

"Nasemaga kila siku kuwa msanii kama msanii usipende kutegemea kufanya 'kolabo' nje ya nchi ndiyo ikufanye wewe utusue kwa sababu muziki ni ule ule, tunasikiliza nyimbo za wazungu hatuelewi maana wanavyoimba lakini tunapenda hits na melody basi.Kwa hiyo mimi ninachoamini ndani ya muziki wangu ninaoufanya naamini ni ladha na napata sms kutoka Nigeria wananisifia muziki wangu mzuri. So nashauri wasanii wenzangu waanze kwanza kufanya muziki wa kitaifa halafu ndiyo washirikishe hao wasanii wa nje,” alisema Nuh Mziwanda.
Nuh Mziwanda- sihitaji kollabo Nuh Mziwanda- sihitaji kollabo Reviewed by Unknown on 01:18:00 Rating: 5

No comments

Recent