Home Top Ad

Responsive Ads Here

Samia kuwashika Everton

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekubali ombi la kuwa mgeni rasmi katika mchezo kirafiki kati ya timu ya Everton ya nchini Uingereza dhidi ya  Gor Mahia ya Kenya iliyotwaa kombe la michuano ya Sportpesa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Watendaji wa Sportpesa.

Mhe. Samia amekubali ombi hilo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa kampuni inayojishughulisha na ubashiri wa michezo ya 'Sports Betting' nchini ambao waliongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji Tarimba Abbas Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na hayo, Makamu wa Rais amepongeza mipango na mikakati mizuri ya kampuni hiyo ya kutaka kukuza vipaji vya wanamichezo hasa kwa mpira wa miguu kwa Tanzania Bara na Zanzibar na kusema kama malengo hayo yatafikiwa Tanzania itakuwa bora katika mchezo huo katika bara la Afrika na dunia kwa ujumla huku akiwataka watendaji wa kampuni hiyo endapo watakwama katika jambo lolote wawasiliane na ofisi yake ili tatizo linalowakabili liweze kutafutiwa ufumbuzi ili lisikwamishe shughuli za kampuni hiyo

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya 'Sports Betting' nchini, Tarimba Abbas amemweleza Makamu wa Rais kuwa kampuni hiyo ina malengo makubwa ya kufanya biashara hapa nchini kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi huku akisisitiza kuwa katika mipango yao wanataka katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, kampuni yao iwe ni moja ya kampuni bora nchini katika ulipaji wa kodi kwa serikali kama wanavyofanya kwa sasa katika serikali ya Kenya.

Tarimba ameongeza kwamba mipango na mikakati waliyonayo kwa sasa ni kuhakikisha wanainua vipaji vya wanamichezo nchini kwa sababu Tanzania Bara na Zanzibar kuna vipaji vingi vya wachezaji wa mpira wa miguu ambavyo haviendelezwi ipasavyo.
Samia kuwashika Everton Samia kuwashika Everton Reviewed by Unknown on 02:29:00 Rating: 5

No comments

Recent