Home Top Ad

Responsive Ads Here

Kikwete avunja rekodi ya mapokezi bungeni

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete leo ameteremsha kishindo cha aina yake bungeni baada ya wabunge kumshangilia kwa muda mrefu huku wengine wakitamka maneno ya kutaka arudi tena madarakani kama itawezekana. 

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na mkewe Mhe. Salma Rashid Kikwete bungeni Dodoma leo.
Kikwete leo alikwenda bungeni kumpa 'suppor't mke wake ambaye aliteuliwa kuwa mbunge na Rais John Pombe Magufuli na leo alikuwa akila kiapo bungeni katika kikao cha kwanza cha mkutano wa saba wa Bunge la 11 ulioanza leo.
Kufutia mapokezi hayo ya aina yake, Spika wa Bunge hilo Job Ndugai amekiri kuwa katika kipindi chote ambacho yeye alikuwa bungeni hajawahi kuona mgeni amepokelewa kwa shangwe kiasi kile. 
"Waheshimiwa wabunge binafsi mimi ni kipindi cha nne humu bungeni sijawahi kuona mgeni amepokelewa kwa kiwango hiki" alisema Spika wa Bunge Job Ndugai ikiwa ni kauli inayomaanisha kuvunja rekodi ya mapokezi katika vipindi vinne vya bunge vilivyopita.
Kwa upande wake Rais mstaafu baada ya kushuhudia kiapo cha mkewe alisema kuwa sasa ni wakati wake yeye kumuunga mkono mkewe kama ambavyo yeye alikuwa akifanya kipindi ambacho alikuwa Rais wa nchi. 
"Leo asubuhi nimeshuhudia kiapo cha Mke wangu Mhe. Salma Rashid Kikwete kuwa Mbunge wa Kuteuliwa Bungeni Dodoma.Ni zamu yangu kumuunga mkono. Nikiwa Bungeni pia nimepata pia fursa ya kusaini kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Marehemu Mhe.Dkt. Elly Macha, Mbunge wa Viti Maalum - CHADEMA" aliandika Mhe. Jakaya Kikwete kwenye ukurasa wake wa twitter 
Kikwete avunja rekodi ya mapokezi bungeni Kikwete avunja rekodi ya mapokezi bungeni Reviewed by Unknown on 03:34:00 Rating: 5

No comments

Recent