Home Top Ad

Responsive Ads Here

Tanzania yapaa kwa nafasi 22 viwango vya FIFA

Tanzania imepaa kwa nafasi 22 hadi nafasi ya 135 kutoka nafasi ya 157 kati ya mataifa 211 katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na FIFA leo Aprili 6, 2017.


Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars
Hivi karibuni, Tanzania katika mechi za kalenda ya FIFA, iliwashinda Botswana na Burundi katika michezo miwili tofauti zilizofanyika Machi, mwaka huu.
Katika viwango hivyo vipya vya mwezi April, Brazil imeishusha Argentina kileleni na kukamata usukani rasmi wa dunia, huku Argentina ikishuka hadi nafasi ya pili na Ujerumani imebaki katika nafasi yake ya 3.
Katika ‘top ten’, mataifa yanayofuata ni Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Uswisi na Hispania inakamata nafasi ya 10
Barani Afrika Misri  inaongoza ikiwa nafasi ya 19 ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 30, Cameroon nafasi ya 33,  Burkina Faso nafasi ya 35, Nigeria nafasi ya 40 na Congo DR nafasi ya 41 ikiwa mbele ya Tunisia kwa nafasi moja
Kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda bado inaongoza ikiwa imepanda kwa nafasi mbili hadi nafasi ya 72, ikifuatiwa na Kenya nafasi ya 78, Rwanda nafasi ya 117,  Ethiopia nafasi ya 124,  Tanzania nafasi ya 135 na Burundi imeshuka kwa nafasi mbili hafasi ya 141.
Wengine ni Djibouti ambayo iko nafasi ya 194 huku Eritrea na Somalia zikiwa mkiani kabisa katika nafasi ya 206
Tanzania yapaa kwa nafasi 22 viwango vya FIFA Tanzania yapaa kwa nafasi 22 viwango vya FIFA Reviewed by Unknown on 11:09:00 Rating: 5

No comments

Recent