Home Top Ad

Responsive Ads Here

Mgomo vyombo vya usafiri 'wayeyuka'

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri na Nchi Kavu na Majini, Sumatra, pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji wamekubaliana kusitisha mgomo wa usafirishaji wa abiria na mizigo uliopangwa kuanza kesho.


Gilliard Ngewe - Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe amesema kusitishwa huko kunatokana na kikao na Waziri wa Mawasiliano Uchukuzi na Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa, kuhusu kuandika kwa kutenganisha makosa ya dereva na wamiliki wa mabasi
Bw. Ngewe amesema, kanuni hizo zitaandikwa ndani ya siku 14 katika rasimu hiyo na wadau wa usafirishaji kuendelea na shughuli za usafirishaji na kwamba, baada ya kufanya marekebisho ya rasimu ya kanuni itarudishwa kwa wadau kuweza kujadiliwa kwa ajili ya kuwasilishwa Bungeni .
Naye Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi, Taboa, Abdallah Mohamed, amesema wamekubaliana na Sumatra kurekebishwa kwa baadhi ya kanuni za makosa kati ya wamiliki na madereva wa mabasi.
Mgomo vyombo vya usafiri 'wayeyuka' Mgomo vyombo vya usafiri 'wayeyuka' Reviewed by Unknown on 03:39:00 Rating: 5

No comments

Recent