Home Top Ad

Responsive Ads Here

Uwezo wa Billnass wamuumbua Jay Moe

Mkongwe wa Hip Hop, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’ ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Nisaidie Kushare’ amekiri kutamani kumuandikia mistari pamoja na kufanya kazi na rapa Billnass kama atakuwa tayari, licha ya kumdharau siku za mwanzo.


Billnas (kushoto) na Jay Moe
Rapa huyo amefunguka hayo hivi karibuni na kudai kuwa kabla ya kusikia kazi za Billnass aliwahi kumdharau lakini baada ya kumuona ametamani kufanya naye kazi kwa kuwa amevutiwa na uwezo wa rapa huyo anayetamba na ngoma ya Mazoea aliyomshirikiaha Mwana FA.
Jay Moe ameongeza kuwa kabla ya kumuona, kusikiliza na kutazama video zake hakuwa akijua uwezo mkubwa alionao rapa huyo hivyo hata alipotumiwa wimbo wa rapa huyo na meneja wake alidharau hakuusikiliza hadi walipokutana nchini Afrika Kusini.
“Unajua kuna siku meneja wake, Billnas ‘Mchafu’, alinitumia wimbo akiniomba niwatumie na wengine lakini mimi sikufanya hivyo, nilipowakuta Afrika Kusini na kuwahoji wakaniambia wapo kwa ajili ya kufanya video ya wimbo alionitumia, nilijisikia vibaya sana na niliona aibu maana niliona video yake ni kali tofauti na nilivyokuwa nikimdhania,” Jay Moe alifunguka
Mkongwe huyo amesema alijifunza kitu kupitia Billnass na kwamba hupaswi kumdharau mtu usiyemfahamu.
"Hapo nikajifunza kitu kuwa hutakiwi kumdharau mtu, maana dogo ana uwezo mkubwa wa kurap na anajua nini anafanya hadi nimemwahidi kufanya naye kazi,”  alisema Jay Moe.
Uwezo wa Billnass wamuumbua Jay Moe Uwezo wa Billnass wamuumbua Jay Moe Reviewed by Unknown on 03:42:00 Rating: 5

No comments

Recent