Home Top Ad

Responsive Ads Here

Serengeti Boys safarini kuelekea 'vitani'

Kikosi cha cha wachezaji 23 cha Serengeti Boys pamoja na viongozi kimeondoka leo kuelekea nchini Morocco kwaajili ya kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na mashindano ya AFCON kwa vijana huku kikiahidi kuitumia kambi hiyo ili kurudisha matumaini Tanzania


Kikosi cha Serengeti Boys kikiwa Uwanja wa Ndege jijini Dar es salaam kwaajili ya maandalizi ya safari ya kuelekea nchini Morocco leo.
Kocha wa timu hiyo Bakari Shime amesema, kikosi chote kipo imara kisaikolojia na amaamini watalipa deni la watanzania kwa kuitumia kambi hiyo vizuri ili kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya AFCON nchini Gabon.
"Vijana wangu wapo imara kisaikolojia na nawaamini wataweza kulipa deni la watanzania kwani najua deni tulilonalo kutokana na sapoti tunayoipata," amesema.
Shime amesema, mpaka sasa wamebakiza mechi takribani nne za kirafiki ili kuhakikisha kikosi kinakuwa imara kwa ajili ya kwenda kupambana nchini Gabon.
"Tulipanga kucheza michezo saba mpaka tisa ya kirafiki na kwa sasa tumeshacheza michezo mitatu hivyo tukiwa katika kambi ya nchini Morocco tutakuwa na michezo miwili na tukienda nchini Cameroon pia tutakuwa na michezo mingine miwili ya kirafiki kabla ya kuelekea nchini Gabon rasmi sasa kwa ajili ya mashindano," amesema.
Kwaupande wake nahodha wa kikosi hicho . Issa Abdi Makame amewataka watanzania kuendelea kuwachangia ili kuongeza morali ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Mei 14 mwaka huu.
"Naimani kambi itakuwa na manufaa makubwa sana kwetu kwani ni nafasi nzuri ya kujiandaa kwa ajili ya kuitangaza zaidi nchi yetu na tunawaomba watanzania waendelee kutuchangia ili kuendelea kutupa morali ya kufanya vizuri zaidi," amesema.
Serengeti Boys safarini kuelekea 'vitani' Serengeti Boys safarini kuelekea 'vitani' Reviewed by Unknown on 11:06:00 Rating: 5

No comments

Recent