Home Top Ad

Responsive Ads Here

Ndugai awatia kikaangoni Mbowe na Mdee

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai ameagiza mbunge wa kawe Halima Mdee, na kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kujitokeza mbele ya kamati ya maadili kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi bungeni.
Katika taarifa yake, Spika Ndugai amesema Mbunge Halima Mdee siku ya juzi wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki alikika akitoa lugha ya matusi, jambo ambalo limewasikitisha wengi ambao wamemtumia ujumbe na yeye kama Spika ameamua kulipeleka suala hilo kwenye kamati ya maadili.

Ndugai amesema huo ni muendelezo wa Bunge hilo kuweka nidhamu ndani na nje ya Bunge miongoni mwa wabunge, ambapo amesema kila mbunge mmoja mmoja atafuatiliwa na kushughulikiwa, huku akitoa tahadhari kwa wabunge wenye tabia ya kutumia lugha zisizo za staha.
"Naanza Halima Mdee, ambaye yeye alimtukana Spika juzi, watanzania wengi wamesikitishwa sana na jambo hili, wameniandikia na kunipigia simu. Na hii si mara ya kwanza kwa Halima, hata juzi nilivumilia sana, nilimuomba Mungu anisaidie nikanyamaza kimya, kwahiyo suala lake nalipeleka mara moja kwenye kamati ya maadili, haiwezekani bunge hili liwaite watu walioko nje kwa utovu wa nidhamu halafu liwafumbie macho wabunge walioko humu ndani, ambao ni watovu wa nidhamu". Amesema Ndugai
Ndugai pia amesisitiza kuwa kama Halima asiporipoti kesho , jeshi la polisi limsake na kumpeleka huku likiwa limefunga pingu "Halima Mdee popote pale alipo najua hayupo Dodoma kesho mida hii awe ameripoti kwenye kamati, , kama asiporipoti akamatwe na polisi popote na aletwe na pingu hapa, tumekuja mmoja mmoja na tutashughulikiana mmoja mmoja"
Kuhusu Mbowe, Spika hajataja tuhuma zinazomkabili, isipokuwa amesisitiza kuwa naye anahitajika kwenye kamati hiyo leo.
Ndugai pia amemuita Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti ambaye bunge hilo katika mkutano wake wa sita liliadhimia aitwe kwenye kamati hiyo kwa tuhuma za kuingilia madaraka ya Bunge.
Ndugai awatia kikaangoni Mbowe na Mdee Ndugai awatia kikaangoni Mbowe na Mdee Reviewed by Unknown on 11:03:00 Rating: 5

No comments

Recent