Baada ya Nape kutolewa bastola, Mwigulu atoa agizo
Baada ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni mbunge wa Mtama kutolewa bastola jana, Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba ametoa agizo kwa IGP
Mh. Mwigulu Nchemba amemuagiza IGP kumshughulikia mtu huyo aliyetoea silaha kumtishia Mh. Nape Nnauye
"Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini".Ameandika Mh. Mwigulu Nchemba
Pia Waziri huyo wa Mambo ya Ndani aliendelea kuandika yafuatayo
"Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake".
Mh. Nape Nnauye alitishiwa na bastola hiyo jana mchana kweupe mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akitaka kuingia katika hotel ya Protea kuzungumza na wanahabari
Baada ya Nape kutolewa bastola, Mwigulu atoa agizo
Reviewed by Unknown
on
00:54:00
Rating:
No comments