Home Top Ad

Responsive Ads Here

Afariki akichaji simu huku akioga kwenye bafu

Mwanamume mmoja alifariki baada ya kupigwa na umeme alipokuwa alichaji simu yake huku akioga kwenye bafu.
Richard Bull, mwenye umri wa miaka 32 alifariki wakati chaji yake ya aina ya iphone ilipoguza maji aliyokuwa akioga nyumbani kwake huko Ealing, mashariki mwa London.
Kifo chake kilitajwa kama kilichotokana na ajali.
Makundi ya kampeni yamekuwa yakiwashauri watu wasichaji simu karibu na maji.
Alipata majeraha ya moto kifuani, na kwenye mkono wake wakati kifaa hicho kilipokaribiana na maji tarehe 11 mwezi Disemba.
Kisa hicho kimechangia kuangaziwa kwa hatari zinazosababishwa na vifaa vya umeme hasa wakati viko karibu na maji.
Idara ya usalama unayosika na kuzuia ajali inawaonya watu ikiwataka wasitumie vifaa vya umeme kwenye bafu.
Afariki akichaji simu huku akioga kwenye bafu Afariki akichaji simu huku akioga kwenye bafu Reviewed by Unknown on 07:11:00 Rating: 5

No comments

Recent