Home Top Ad

Responsive Ads Here

FIFA yaidhinisha kuwepo timu 48 kombe la dunia

Chama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa michezo sita ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia mwaka 2020.
FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo.
Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema.

Mchakato huo utakuwaje?

Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.
Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali.

Mapendekezo hayo yapo hivi

Afrika - 9 kutoka timu za awali 5
Asia - 8 kutoka timu 4 za awali
Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali
Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali
Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali
Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali
Mwezi januari chama hicho chenye mamlaka makubwa ya soka duniani, kilipanga kuongeza timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia kutoka 32 mpaka 48 na hii itaanza mwaka 2026.
FIFA yaidhinisha kuwepo timu 48 kombe la dunia FIFA yaidhinisha kuwepo timu 48 kombe la dunia Reviewed by Unknown on 00:01:00 Rating: 5

No comments

Recent