Ndege ya ‘wanawake pekee’ kutoka Malawi kutua Tanzania
Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limetangaza kwamba linapanga kufanya safari ya ndege itakayosimamiwa na wanawake pekee Alhamisi wiki hii.
Safari hiyo ya ndege, ambayo itakuwa na marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege wote wakiwa wanawake, itakuwa ya kwanza kuandaliwa na shirika hilo.
Ndege hiyo itasafirisha abiria kutoka mji wa Blantyre hadi Dar-es-Salaam nchini Tanzania na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar .
Taarifa kutoka kwa shirika hilo la ndege, lilisema lengo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".
Ndege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.
Bi Mwenifumbo, 24, alisomea taaluma ya uchukuzi wa ndege mjini Addis Ababa, Ethiopia.
"Lengo la hatua hii ni kuwahamasisha wasichana ambao wangependa kufanya kazi katika uchukuzi wa ndege lakini kwa njia moja au nyingine hufikiria ni vigumu au kwamba ni kazi ambayo wanawake hawaiwezi," taarifa ya Malawi Airlines ilisema.
Ndege hiyo aina ya Bombardier Q-400 itapaa kutoka Blantyre saa nne asubuhi Alhamisi.
Ndege ya ‘wanawake pekee’ kutoka Malawi kutua Tanzania
Reviewed by Unknown
on
03:39:00
Rating:
No comments