Home Top Ad

Responsive Ads Here

Serengeti Boys nao 'waigonga' Burundi

Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys, lwamefuata nyayo za kaka zao 'Taifa Stars' kwa kuipiga timu ya vijana Burundi na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.


Mchezo huo umepigwa katika dimba la Kaitaba Mjini Bukoba, na ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kuelekea katika michuano ya Afrika kwa vijana itakayofanyika nchini Gabon mwezi Mei 14 mwaka huu..
Katika mchezo wa leo ambao ni wa kwanza kati ya michezo mitatu, Serengeti Boys wameonesha kiwango cha hali ya juu dhidi ya wapinzani wao na kufanikiwa kupata mabao hayo kupitia kwa Hussein Makame dakika 20, Kibabage dakika ya 38 na Yohana Nkomola akipiga bao la 3 dakika ya 72 kwa njia ya penati.
Timu hiyo inatarajia kukutana tena na Burundi katika mchezo wake wa pili wa kirafiki katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kabla ya kuwasili jijini Dar es salaam kupambana na Ghana na mara baada ya mchezo huo itaondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya fainali za AFCON kwa vijana
Serengeti Boys nao 'waigonga' Burundi Serengeti Boys nao 'waigonga' Burundi Reviewed by Unknown on 23:52:00 Rating: 5

No comments

Recent