Home Top Ad

Responsive Ads Here

Uchunguzi kuhusu kavamiwa studio za Clouds Media kuanzishwa. "NAPE MNAUYE"

Waziri wa habari nchini Tanzania Nape Nnauye, ameanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo kituo kimoja cha runinga kilivamiwa na mtumishi wa serikali.
Kamera za CCTV katika kituo hicho zinamuonyesha mkuu wa mkoa wa jiji la Dar es Salaam Paul Makonda (mwenye kofia), akiwa anasindikizwa na polisi waliojihami, akiingia studio za Clouds Media Group siku ya Ijumaa usiku.
Wakitoa malalamishi yao kupitia kwa mitandao ya kijamii, watu wamekuwa wakimtaka Mkuu wa mkoa  huyo kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Ripoti zinasema kuwa bwana Makonda hakufurahishwa kuwa kituo hicho kilishindwa kupeperusha taarifa za kumchafulia jina kiongozi mmoja wa dini kwa jila la Gwajima wa kanisa la ufufuo.
Bwana Makonda na kiongozi huyo wa dini,wametofautiana hadharani kuhusu kile kichotajwa kuwa sakata ya madawa ya kulevya.
Uchunguzi kuhusu kavamiwa studio za Clouds Media kuanzishwa. "NAPE MNAUYE" Uchunguzi kuhusu kavamiwa studio za Clouds Media kuanzishwa. "NAPE MNAUYE" Reviewed by Unknown on 04:29:00 Rating: 5

No comments

Recent