Home Top Ad

Responsive Ads Here

Harmorapa asimulia kilichomtoa mbio kwa Nape

Msanii asiyekaukiwa 'kiki' katika ulingo wa sanaa ya Bongo, Harmorapa amesimulia kilichomkuta alipokwenda kumuona aliyekuwa Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kiasi cha kutoka mbio za aina yake, baada ya kuona bastola. 

Harmorapa ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la 'Kiboko ya Mabishoo' aliyomshirikisha Juma Nature, amesema kilichomfanya aende katika mkutano ule mara baada ya Nape kuondolewa kwenye nafasi yake ya uwaziri, ni kumpa pole na kumshukuru Nape kwa kuwa ndiye aliyekuwa mlezi wa tasnia ya sanaa nchini.
Akizungumzia tukio alilolishuhudia la Nape kutishiwa bastola mbele yake, Harmorapa  amekiri kuwa ni kweli hajawahi kuiona kwa ukaribu ule, hivyo alipoona inachomolewa aliogopa na kujikuta akitoka mbio, huku akikanusha utani ulioenea mitandani kuwa alikimbia hadi Mtwara.

Harmorapa asimulia kilichomtoa mbio kwa Nape Harmorapa asimulia kilichomtoa mbio kwa Nape Reviewed by Unknown on 00:49:00 Rating: 5

No comments

Recent