Squeezer asema Muziki wa sasa una ladha ya bubble gum
Mwanamuziki mkongwe katika anga la bongo fleva Squeezer amefunguka juu ya muziki unaofanywa na vijana wengi wa sasa kwamba hauwezi kudumu kwani wengi wanaokimbilia kufanya sanaa hiyo hawana ubunifu wa kutosha.
Leo Squeezer amese kwamba aina ya muziki wanaofanya vijana wa sasa una ladha ya peremende ambayo inadumu kwa muda mfupi hasa ikipewa nafasi kubwa ya kusikika masikioni mwa watu zinakera.
"Nyimbo pamoja na wasanii wengi wa sasa wapo mbioni kupotea kutokana na kuwa na ubunifu mdogo sana katika kazi zao, wengi hawana 'knowledge' ya kutosha. Wanatunga nyimbo zenye ladha ya 'bubble gum' mtaani wanaziita hivyo kwa kuwa haziwezi kudumu zaidi ya miezi miwili. na nyie watangazaji mnavyozipa muda hewani ndo zinakuwa hata mwezi haziwezi kusurvive". Squeezer alisema.
Msanii huyo ameongeza kwa kuwashauri wasanii warudi shule ili kupata uelewa katika kuboresha kazi zao na kusisitiza kwamba kama ni muziki upo kila siku na siku zinavyozidi kwenda hela zinazidi kuwa nyingi na kunamuongezea heshima msanii.
Squeezer aliyewahi kutamba na ngoma iitwayo 'Naja' aliyomshirikisha Juma Nature amesema huo ndiyo wimbo uliompatia mashabiki wengi ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na mafanikio mengi.
Squeezer asema Muziki wa sasa una ladha ya bubble gum
Reviewed by Unknown
on
11:20:00
Rating:
No comments