Home Top Ad

Responsive Ads Here

Mdee kuendelea kusota lupango

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kumshikilia msanii wa muziki wa bongo fleva Vanessa Mdee a.k.a Vee Money kwa tuhuma za kuhusika na matumizi ya dawa za kulevya.


Kamanda wa Jeshi hilo, Kamishna Simon Sirro amesema kwa taarifa walizonazo, msanii huyo pamoja na watuhumiwa wengine, wanahusika na matumizi pamoja na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Sirro amesema msanii alikamatwa juzi jijini Dar es salaam, na upelelezi unaendelea.
"Tunamshikilia msanii Vanessa Mdee tangu Jumatano ambaye taarifa zinaonyesha kuwa ni mtumiaji lakini pia ni msambazaji wa dawa za kulevya, tunaendelea na uchunguzi wetu na tukikamilisha uchunguzi wetu na ikathibitika kama ana kosa la kujibu basi, tutamfikisha mahakamani". Amesema Sirro
Mdee kuendelea kusota lupango  Mdee kuendelea kusota lupango Reviewed by Unknown on 01:01:00 Rating: 5

No comments

Recent