Home Top Ad

Responsive Ads Here

Ay na FA watupiana vijembe, Ridhiwani Kikwete alitabiri matokeo ya BARCELONA

Kati ya mashabiki maarufu wa timu ya Barcelona hapa nchini ni msanii wa kizazi kipya Ambwene Yessaya almaarufu kama AY.Furaha ya AY haikuisha jana usiku kwani hadi saa hizi amekuwa akishindwa kuzificha hisia zake huku akiendelea kumtania mtani wake na rafiki yake wa karibu Mwana FA.
Mwana FA ambaye ni mtu wa karibu wa AY amekuwa akiishambulia Barcelona ambayo ni timu ya AY akidai kwamba wamebebwa.FA anapinga Barcelona kupewa penati mbili na AY amemjibu Mwana FA kwa kumuambia kama anaona magoli hayo siyo ya halali baasi akayatoe.Mwana FA hakubaki nyuma baada ya kuabiwa hivyo na AY aliibuka tena na kumjibu AY kwamba hayo magoli ya kubebwa yakitolewa baasi Barcelona nao wanatoka.
AY leo asubuhi tu kulipokucha aliibuka na moja ya mstari maarufu wa Mwana FA unaosema “kuzoea zoea watu mwisho utazoea majini”.Lakini AY yeye akasema “kucheza cheza na timu mwisho mtacheza na majini” kauli ambayo ni kama onyo kwa wote ambao watakabiliana na Barcelona.AY anaifananisha Barcelona na majini walioshindikana na kiasi kwamba ni ngumu kuwasimamisha.
AY leo asubuhi alitupa kijembe kingine kwa wapinzani wao akisema wanatamani usiku uwe mrefu asubuhi isifike.Kama hiyo haitoshi AY alimrudia tena Mwana FA na kumuambia matani aliyojiandaa kumtania AY sasa ajitanie mwenyewe.Ni kama AY alipania kumnyamazisha kabisa FA kwani alimuambia wao wamefunga goli sawa na nafasi ya Man United katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.
Kabla ya mchezo kuanza mshabiki mwingine mkubwa wa Barcelona nchini Tanzania ambaye ni mtoto wa zamani wa raisi wa Tanzani na pia ni mbunge wa Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alisema yake.Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ridhiwani alipost picha akiwa kwake na jezi yake ya Barcelona.Katika picha hiyo Ridhiwani aliandika: “Niko tayari kuithibitishia dunia kuwa sisi ni kiboko.”
Baada ya post hiyo kuliibuka kundi la mashabiki wasioipenda Barcelona.Wengi walionekana kumpa pole huku wengine wakimuambia ajiandae kwa msiba wa Barcelona,Ridhiwani aliwajibu kwa kuwaambia “nyie chongeni mimi nafanya yangu” lakini hivi sasa wengi wanampongeza kwa matokeo ya jana.
Ay na FA watupiana vijembe, Ridhiwani Kikwete alitabiri matokeo ya BARCELONA Ay na FA watupiana vijembe, Ridhiwani Kikwete alitabiri matokeo ya BARCELONA Reviewed by Unknown on 05:30:00 Rating: 5

No comments

Recent