Home Top Ad

Responsive Ads Here

Sihitaji 'kiki' kutoa 'hit' - Maua Sama

Mwanadada anayetamba na ngoma ya Main Chick, Maua Sama amesema yeye hategemei 'kiki' ili ku-'hit' bali uzuri wa kazi zake, na kuwataka wasanii wengine waache kutafuta 'kiki' ili kupata majina bali wajikite kwenye kutengeza kazi nzuri.


Maua amesema kuwa wasanii wengi wamejikita kwenye kutafuta kiki badala ya kuwapa mashabiki ladha tofauti na kusisitiza kwamba dhana ya kiki inapaswa kufutika ili kila mtu afanye kazi nzuri.
"Ukifanya muziki mzuri lazima tu utapata jina, wala hakuna haja ya kiki, mfano mzuri mimi hapa ni msanii ambaye nimepata sapoti nzuri sana kwenye 'game' bila kuongelewa kwa mambo mabaya ya kiki, 'The real deal is good music' siyo skendo, japo mimi nina skendo ya kutoa ngoma kali siku zote". Maua aliwaambia Dullah na Jay R watangazaji wa kipindi hicho.
Sama ameongeza kwamba katika muziki wapo wasanii ambao wanafanya muziki mbaya lakini wanapewa nafasi kubwa ya kusikilizwa kutokana na kiki lakini hana chuki nao kwani pia watu wa aina hiyo wana mashabiki zao wanaopenda kuwasikiliza.
"Mimi nina wivu wa maendeleo sana, lakini sina chuki na watu wanaofanya muziki mbaya kwani hata wao wana masoko yao na wanauza ila kinachotokea kwangu nikimuona mtu katoa kazi mbaya mimi naingia kutengeneza 'hits' kali ili nipate soko zaidi". aliongeza Maua.
Hata hivyo Maua ameongeza kuwa msanii yoyote ambaye huandika nyimbo zake kipindi anapokuwa kwenye hisia yoyote ni wazi wimbo huo ukiachiwa hewani lazima uwe mkali kwa kuwa unakuwa umebeba uhalisia na hisia za kweli.
Sihitaji 'kiki' kutoa 'hit' - Maua Sama Sihitaji 'kiki' kutoa 'hit' - Maua Sama Reviewed by pongwa trading on 00:59:00 Rating: 5

No comments

Recent