Home Top Ad

Responsive Ads Here

Mahakama yatengua hukumu ya kifungo kwa Mbunge

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuachia huru mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Peter Lijualikali.

Mbunge wa Kilombero - Peter Lijualikali
Lijualikali amekutwa hana hatia katika kesi ambayo alihukumiwa kifungo cha miezi sita na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero kwa kosa la kufanya vurugu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mawakili wake wakiongozwa na na Tundu Lissu walikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo na leo imebainika kuwa mbunge huyo alikuwa hana hatia.
Januari 11 mwaka huu Mahakama ya wilaya ya Kilombero ilimuhukumu kifungo cha miezi sita jela Mbunge Lijualikali kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Mahakama yatengua hukumu ya kifungo kwa Mbunge Mahakama yatengua hukumu ya kifungo kwa Mbunge Reviewed by Unknown on 23:56:00 Rating: 5

No comments

Recent