Home Top Ad

Responsive Ads Here

RUGE MUTAHABA afafanua juu ya sakata la uvamizi CLOUDS FM

leo machi 20, 2017 Mkurugenzi wa clouds media group RUGE MUTAHABA  aweka wazi juu ya suala linaloendelea katika taasisi hiyo ya utangazaji na uzalishaji mali.

RUGE MUTAHABA amesema sakata lilianza kama masihara sana, 
siku ya alhamisi alipigiwa simu na mchungaji GWAJIMA kumueleza kuhusu sakata hilo mpaka kufikia tarehe 19 mwezi machi ambapo ndipo sakata hilo lilisambaa mitandaoni.

bwana ruge mutahaba asema ni jambo lililotokea kweli kwa vijana wake wa kipind cha shilawadu. na hata ivyo ruge alimpigia simu mkuu wa mkoa Paul makonda na kumuuliza mbona ameenda ofisini usiku kuna nini na mkuu wa mkoa kujibu kwa nini umezuia kipindi changu?

pia Ruge amesema hakujeruhiwa mfanyakazi yeyote yule siku hiyo na anakili urafiki wao ndio chanzo kikubwa kuzoena mpaka kufikia hivyo.

nilitegemea ataomba msamaha rakini mpaka leo hii hajaomba msamaha wala nini....makonda ni mdogo wangu hata kama ni mkuu wa mkoa.....alisema ruge.

kuhusu suala la kufungua mashitaka bado hatafanya maamuzi lakini waandishi wenzetu na wanahabari wenge wananipigia simu ili kufahamu kinachoendelea na kuchukua hatua lakin wao hawawezi chukua hatua yeyote ile kwanza kuhusu kufungua mashitaka mpaka clouds iongee


pia amesema vijana wake wapo katika hali mbaya sana kiamani kufuatia na tukio hilo lililotokea.

na pia amewaomba wananchi hili jambo liishe leo na kuendelea na kampeni zingine za malikia wa nguvu.

lakini richa ya hayo yote wao wapo tayari kushilikiana na serikali kwa kila jambo kwani ni masilahi ya wananchi kwa ujumla 


RUGE MUTAHABA afafanua juu ya sakata la uvamizi CLOUDS FM RUGE MUTAHABA afafanua juu ya sakata la uvamizi CLOUDS FM Reviewed by Unknown on 02:07:00 Rating: 5

No comments

Recent