Home Top Ad

Responsive Ads Here

Msimamo wa VPL baada ya mechi ya Ruvu Shooting vs Yanga

Baada ya mchezo wa jana wa kiporo kupigwa na Yanga kuibuka na pointi tatu kwa kuifunga Ruvu Shooting 2-0, Yanga imejiongezea alama tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara lakini hakuna mabadiliko makubwa kwenye msimamo huo ambao Simba SC ndio vinara hadi sasa.
Pointi tatu walizozipata jana Yanga zinafanya wafikishe pointi 52 pointi mbili nyuma ya Simba ambao wanapointi 54 huku timu hizo mbili zinazochuana kuwania ubingwa zikiwa zimecheza mechi 23 hadi sasa.
Vilabu hivi ambavyo vinawania taji la ligi msimu huu vyote kwa pamoja vimepoteza mechi tatu, Simba imetoka sare mara tatu Yanga wao wakiwa wametoka sare katika mechi nne, Simba wameshinda mechi zao 17 wakati Yanga wameshinda michezo 16 hadi sasa.
Vita ni kubwa kati ya vilabu hivi kuwania ubingwa wa ligi msimu huu zikiwa zimesalia mechi saba (7) kuhitimisha msimu wa ligi 2016/17.
Azam FC msimu huu hawako kwenye kinyang’anyiro cha ligi kwa sababu wameachwa kwa idadi kubwa ya pointi na vilabu vya Simba na Yanga. Azam imeachwa pointi 13 na Simba wanaoongoza ligi huku wakiwa pointi 11 nyuma ya Yanga, alama hizo ndio zinafanya Azam kuondolewa kwenye mbio za ubingwa msimu huu kutokana na kasi yao ukilinganisha na kasi ya Simba na Yanga.
Msimamo wa VPL baada ya mechi ya Ruvu Shooting vs Yanga Msimamo wa VPL baada ya mechi ya Ruvu Shooting vs Yanga Reviewed by pongwa trading on 03:43:00 Rating: 5

No comments

Recent