Nape kuwateua wasanii wakongwe DIAMOND na ALIKIBA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema atahakikisha anasaidia kupata vyanzo vya fedha vya kuaminika ili kuhakikisha safari na ushiriki wa michezo mingi zaidi katika Olimpiki 2020 jijini Tokyo, nchini Japan inafanikiwa.
Waziri Nape Nnauye ameyazungumza hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokutana na wadau wa michezo nchini kupanga mikakati ya ushiriki wa soka kwenye mashindano ambapo ameutaka ushiriki wa serikali katika kusaidia soka nchini ikiwa ni pamoja na kufanya mchezo huo kuwa jambo la nchi ili kuukuza na kutangaza zaidi.
"Olimpiki tunaenda kama Watanzania na siyo kama timu pekee hivyo tunatakiwa tushikamane pamoja na kuhakikisha tunashinda pamoja, na ninaposema tunatakiwa kufanya soka kuwa jambo la nchi namaanisha kuwa itasaidia ili hata watu waliokabidhiwa dhamana wakubali kujisahihisha pale wanapokosea, " amesema Waziri huyo.
Nape amewataka pia wadau wa soka na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kuiunga mkono Serengeti Boys katika mashindano ya Afrika nchini Gabon ili ifanye vizuri na kuwa kama sehemu ya mtaji wa kwenda Olimpiki 2020 jijini Tokyo, nchini Japan inafanikiwa.
Katika kuhakikisha Serengeti Boys inafanya vizuri, Waziri Nape ametangaza kamati ya watu 10 wakiwemo wasanii Diamond na Alikiba. Wengine waliomo kwenye kamati hiyo ni pamoja na Celesitne Mwesigwa, Beatrice Singano, Charles Hillary ambaye ndiye anakuwa mwenyekiti, Maulid Kitenge, Ruge Mutahaba na Eric Shigongo.
Katika mikakati yake pia Nape ametangaza rasmi kurejesha michezo ya UMISETA kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
Nape kuwateua wasanii wakongwe DIAMOND na ALIKIBA
Reviewed by pongwa trading
on
03:06:00
Rating:
No comments