Home Top Ad

Responsive Ads Here

Uwoya awachana wasanii wanaodai kulipwa na CCM

Msanii Irene Uwoya amekerwa na kitendo cha wasanii wenzake kutumia vyombo vya habari vibaya kwa kutangaza kuwa walilipwa pesa zao za kampeni kipindi cha uchaguzi mwaka 2015 na kuacha kufanya mambo yenye tija ndani ya jamii.

Uwoya ameandika katika ukurasa wake ya instagram kuwa kitendo hicho ni kujishushia heshima na kutaka vitu vingine vibaki kwa wanaohusika tu sio lazima kuongea kila kitu maana watu wanatamani muda mwingine kusikia vitu ambavyo wanahisi vina faida na sio kila saa kuongelea mambo ya chama.
"Kuna vitu vinaboa sana, kweli kada mzima wa CCM unasimama hadharani unasema tulilipwa kufanya 'campaign' ?, hata kama lakini unafundisha nini jamiii?. Unafundisha jamiii kwamba yote tuliyoongea kuhusu CCM hatukuyamanisha ni kwasababu tulilipwa? unaiambia jamiii ulikuwa mnawadanganya sababu mlilipwa?". Ameandika Irene Uwoya
Aidha msanii huyo amewashauri wenzake wajifunze kunyamaza muda mwingine kama hakuna ulazima wa kuongea maana wanaweza kuhisi wanajenga kumbe ndiyo wanaharibu kabisa.
"Embu tufanye kazi zinazotuhusu jamanii, 'Nigeria' wenzetu sasa wako 'Hollywood' wanaigiza huko sisi hata 'Nigeria' kwenyewe bado hatuja pasua". Ameandika kwa kusisitiza msanii huyo
Irene amewasisitizia wasanii wenzake waache kushabikia ujinga na vitu visivyokuwa na msaada kwa jamiii na kuwataka wapige kazi ili waweze kutoboa ndani ya tasnia yao  vinginevyo wataishia kuiona 'Hollywood' katika televisheni.
Huu ndiyo ujumbe wake...

Uwoya awachana wasanii wanaodai kulipwa na CCM Uwoya awachana wasanii wanaodai kulipwa na CCM Reviewed by pongwa trading on 02:59:00 Rating: 5

No comments

Recent