Home Top Ad

Responsive Ads Here

Azam kukipiga na klabu ya Zambia

Mabingwa wa soka Afrika mashariki na kati na kombe la Mapinduzi (Azam FC) wametangaza kucheza mchezo wa pili wa kimataifa wa kirafiki ambao utawasaidia katika maandalizi yao ya michuano ya kombe la sjhirikisho barani Afrika CAF.
Azam FC tayari wameshacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika na Afrika kusini Mamelod Sondown na kulazimisha sare ya bila kufungana, wamepanga kupambana na klabu ya Red Arrows ya nchini Zambia.
Afisa habari wa Azam FC Jaffari Iddy amesema mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki utapigwa kesho katika uwanja wa Azam Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Amesema Resd Arrows wapo nchini wakijiandaa na ligi ya nchini kwao Zambia na wamekua wakifanya mazoezsi yao katika uwanja wa Azam Complex tangu walipowasili mwishoni mwa juma lililopita.
“Kwa faida na mwendeleo wa soka duniani, tumekubali kuwaruhusu kutumia miundo mbinu yetu kama Azam FC na vilevile kujenga uhusiano , leo tupo Tanzania hatujafungiwa mipaka kuna siku tunaweza kutoka kwenda Zambia kwa ajili ya mchezo wa klabu bingwa au kombe la shirikisho hawa wanaweza kuwa wenyeji wetu na kutusaidia mambo mbalimbali ya kisoka.”
“Tuliwapa nafasi ya kuutumia uwanja wetu tangu wamefika na wanautumia kwa ajili ya mazoezi, kwetu mchezo dhidi ya Red Arrows ni muhimu kwetu Azam kwa sababu tunakabiliwa na mechi za kimataifa kwa hiyo utawasaidia walimu kuweza kuona timu yetu ina mapungufu kiasi gani.”
Kwa upande wa meneja wa timu ya Red Arrows FC Meja Milunga amesema wamefurahishwa na mpango wa uwepo wa mchezo wa kesho ambao wanaamini utawasaidia kuwatimizia jukumu la kujiandaa na mshike mshike wa ligi kuu ya soka nchini Zambia ambayo itaanza baadae mwaka huu.
Meja Milunga pia akatoa sababu za kuichagua Tanzania kwa ajili ya maandalizi yao ya msimu mpya wa ligi ya Zambia, kwa kusema hali ya hewa pamoja na uwepo wa miundombinu ilikua sababu ya uongozi wao kuafiki kikosi cha Red Arrows kuweka kambi katika jiji la Dar es salaam.
Mechi ya Azam vs Red Arrows iachezwa kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 1:00 usiku.
Azam kukipiga na klabu ya Zambia Azam kukipiga na klabu ya Zambia Reviewed by Unknown on 11:07:00 Rating: 5

No comments

Recent