Home Top Ad

Responsive Ads Here

Makamanda wa jeshi wajiuzulu Sudan Kusini

Maafisa watatu wakuu wa kijeshi ndani ya serikali ya Sudan Kusini, wamejiuzulu.
Makamanda hao wamejiondoa serikalini wakimlaumu Rais Salva Kiir kwa kuhusioka katika uhalifu wa kivita na mauwaji yanayolenga kabila fulani.

Brigedia Henry Oyay Nyago, anamshutumu Rais, ambaye anatoka katika kabila la Dinka, kwa kuamuru kuwawa kwa watu wasiotoka katika kabila hilo la Dinka.
Kanali Khalid Ono Loki, pia anamlaumu kiongozi mkuu wa jeshi kwa mauwaji ya kimbari, kukamatwa na kuwazuilia watu kiholela.
Makamanda wa jeshi wajiuzulu Sudan Kusini Makamanda wa jeshi wajiuzulu Sudan Kusini Reviewed by pongwa trading on 00:54:00 Rating: 5

No comments

Recent