Home Top Ad

Responsive Ads Here

Trump ampigia simu Xi Jinping na kukubali msimamo kuhusu China

Rais wa Marekani Donald Trump amekubali kuheshimu kile anachokiita sera ya "China Moja" pale alipompigia simu Rais wa China Xi Jinping, Ikulu ya White House imesema.
Sera ya China Moja ni elimu ya kidiplomasia, kwamba kuna serikali moja tu iitwayo China.
Bwana Trump alitilia shaka sera ya muda mrefu ya china, pale alipofanya mazungumzo na Rais wa Taiwan ,mwezi Desemba.
Hiyo ni mojawepo ya hatua kubwa mno ya kuvunja tamaduni ya muda mrefu ya kufuata taratibu ya uongozi, na kuchochea malalamiko rasmi kutoka kwa utawala wa China.
Mazungumzo hayo ya simu ni ya kwanza kati ya marais hao wawili tangu Trump alipoingia ofisini Januari 20, licha ya Rais Trump kuwapigia simu viongozi wa mataifa kadhaa duniani.
Ikulu ya White House inasema kuwa maswala mbalimbali yalijadiliwa wakati wa mazungumzo hayo ya simu ambayo ilitajwa kama " mzuri sana ".
Viongozi hao wawili walialikana kuzuru mataifa yao, inasema taarifa hiyo, huku wakitarajia kuendeleza zaidi mazungumzo yao.
Taarifa kutoka Beijing zinasema kwwamba, China inampongeza Bw Trump kwa kutambua sera ya China Moja.
Mataifa haya mawili "washirika wa karibu, na kupitia juhudi za pamoja, tunaweza kuboresha Zaidi uhusiano huu na kufikisha katika kiwango cha juu zaidi katika historia", Taarifa hiyo ilimnukuu Bw Xi.
Mazungumzo hayo ya simu yalifuatia barua iliyotumwa na Bw Trump kwa Rais Xi hapo jana Ahlamisi- hatua ya kwanza ya Trump kumfikia kiongozi huyo wa China.
China imekashirishwa na maoni ya Trump kuihusu Taiwan

Awali Bw Trump alisababisha taharuki kubwa mno na Beijing, wakati alipokubali mawasiliano ya simu kutoka kwa kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-wen.
Hata ingawa Marekani ni mshirika wa karibu wa kijeshi na Taiwan, hakuna Rais au Rais mteule wa Marekani amewahi kuzungumza moja kwa moja na kiongozi wa Taiwan, kwa miongo kadhaa.


Trump ampigia simu Xi Jinping na kukubali msimamo kuhusu China Trump ampigia simu Xi Jinping na kukubali msimamo kuhusu China Reviewed by Unknown on 22:38:00 Rating: 5

No comments

Recent