Home Top Ad

Responsive Ads Here

CHELSEA yazidi kuwa tishio kwa Pep Gurdiola

Baada ya ushindi wa magoli mawili kutoka kwa Raheem Sterling na lile la kujinga la Fc Bournamouth iliwapeleka Man City hadi nafasi ya pili ya ligi ya Uingereza.Man City kwa sasa wanakuwa na alama 52 ikiwa ni alama 8 tu nyuma ya vinara wa ligi hiyo timu ya Chelsea.
Pamoja na ushindi huo lakini Pep Gurdiola haamini kama timu yake itawakuta Chelsea.Ni kama Gurdiola haamini kama Man City wanaweza kuwa mabingwa msimu huu.Pengo la pointi 8 na vinara wa ligi linaonekana sio kubwa sana lakini kocha wa Man City kwa upande wake anaona jinsi Chelsea wanavyocheza ni ngumu kuwakamata.
“Nafurahi tulivyocheza na matokeo tuliyoyapata,imetutoa kutoka nafasi ya tano hadi nafasi ya pili ni jambo jema kwetu,ni vyema zaidi kufuzu champions league msimu ujao,Chelsea walishindwa kupata alama 3 katika mechi yao iliyopita lakini ukiwaangalia wanavyocheza ni ngumu kuwazuia haswa tofauti ya alama tulizonazo na wao” alisema Gurdiola.
Pamoja na kushinda mchezo huo lakini Gurdiola alishuhudia mshambuliaji wake Gabriel Jesus akitoka uwanjani dakika ya 13 na nafasi yake kuchukuliwa na Sergio Aguero.Baada ya mchezo Pep Gurdiola alimmwagia sifa kem kem mshambuliaji wake huyo akisema ni mpambanaji na kiwango alichoonesha kimedhihirisha ni jinsi gani Man City wanamhitaji Aguero.
“Nafurahi kumuona Aguero akicheza hivi,ni mpambanaji na ameonesha ni jinsi gani alivyo muhimu kwetu,hii ni mara ya kwanza katika mwaka huu tunatawala mchezo mzima,tulifanya hivyo mwanzo wa msimu lakini kuna kitu tulipoteza,najua ni kwa nini ila toka mchezo wetu na Arsenal na ule na Totenham tumekuwa tukicheza vizuri” alisema Pep Gurdiola.
CHELSEA yazidi kuwa tishio kwa Pep Gurdiola CHELSEA yazidi kuwa tishio kwa Pep Gurdiola Reviewed by pongwa trading on 11:03:00 Rating: 5

No comments

Recent