Home Top Ad

Responsive Ads Here

Mavazi ya bikini yasababisha maonyesho kupigwa marufuku Guinea

Serikali Guinea imepiga marufuku kwa muda maonyesho ya urembo baada ya mavazi ya bikini kuzua shutuma nchini humo.
Wagombea walijipanga mbele ya waziri mkuu Mamady Youla wakiwa wamevaa bikini siku ya Jumamosa na kasababisha shutuma kwenye mitandao ya kijamii.
Gazeti moja liliandika likiuliza ikiwa waziri mkuu alikuwa akiunga mkono ukahaba.
Waziri wa tamaduni anasema kuwa marufuku hiyo itasalia hadi pale vipengee vipya vya maadili vitatangazwa.
Amasema kuwa kamati imebuniwa kuandika viprngee hivyo.
Pia amesema kuwa serikali imefuta mikataba na waandalizi wa maonyesho hayo ya urembo.

Mavazi ya bikini yasababisha maonyesho kupigwa marufuku Guinea Mavazi ya bikini yasababisha maonyesho kupigwa marufuku Guinea Reviewed by Unknown on 02:25:00 Rating: 5

No comments

Recent