Home Top Ad

Responsive Ads Here

Somalia: Hakuna ndege kuruka Mogadishu siku ya uchaguzi

Somalia imesitisha safari za ndege zinazoingia na kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Mogadishu, siku ya Jumatano ambapo uchaguzi wa Rais utafanyika.
Ikiwa ni wa kwanza kufanyika katika kipindi cha miaka 25.
Mahala uchaguzi utakapofanyika ulihamishwa kutoka katika makao makuu ya polisi hadi katika uwanja wa ndege kutokana na sababu za kiusalama.
Waziri wa Usafiri Ali Jama Kangali ameiambia BBC kwamba hakuna ndege zitakazoruhusiwa katika uwanja wa Mogadishu, siku hiyo ya Jumatano wakati uchaguzi ukiendelea.
Kumekuwa na wasiwasi kwamba wapiganaji wa Al Shabaab wanaweza kufanya mashambulio kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo.
Wapiganaji hao kwa sasa wamekuwa wakiwalenga na kuwaua wanasiasa, raia na wanajeshi kwa kutumia risasi na milipuko. Wamekuwa wakiipinga serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Wabunge 329 wa Somalia watamchagua rais mpya wa nchi hiyo kati ya wagombea 24 wanaowania kiti hicho.
Hali ya kutokuwepo na usalama imesababisha kushindwa kwa watu wote nchini humo kupiga kura kumchagua rais.

Somalia: Hakuna ndege kuruka Mogadishu siku ya uchaguzi Somalia: Hakuna ndege kuruka Mogadishu siku ya uchaguzi Reviewed by Unknown on 02:26:00 Rating: 5

No comments

Recent