Home Top Ad

Responsive Ads Here

mnyama SIMBA arudi kileleni

Simba imerudi kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons na kufikisha pointi 51 pointi mbili zaidi ya Yanga ambayo bado inamchezo mmoja mkononi.
Magoli ya Simba yamefungwa na Juma Liuzio ambaye alifunga goli la kwanza dakika ya 18 baada ya mabeki wa Prisons kuzembea kuondoa mpira kwenye hatari wakidhani Liuzio alikua ameotea.
Ibrahim Ajibu akafunga goli la pili dakika 10 baadae akitumia kwa ustadi pasi aliyowekewa na Laudit Mavugo kabla ya kupasia kamba.
Dakika ya 57 Laudit Mavugo akapiga msumari wa tatu safari hii Ajibu akipiga pasi ya mwisho iliyotua kichwani kwa Mavugo.
Simba mechi mbili magoli 6
Simba imefanikiwa kufunga magoli 6 katika mechi mbili mfululizo. Mchezo uliopita Simba ilishinda ugenini kwa kuifunga Majimaji goli 3-0 ambapo leo wamepata ushindi kama huo.
Ajibu, Mavugo, msmbo safi
Washambuliaji hao wa Simba wamefanikiwa kufunga mfululizo kwenye mechi mbili, walifunga goli moja kila mmoja katika mchezo dhidi ya Majimaji kitu ambacho wamekifanya leo.
Ajibu amefunga goli kwa msaada wa Mavugo huku Mavugo pia akifunga kwa assist ya Ajibu.
Simba imelipa kisasi kwa Tanzania Prisons
Mchezo wa November 9, 2016 uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Prisons waliigaragaza Simba kwa kipigo cha magoli 2-1. Kwahiyo ushindi wa Simba 3-0 Prisons ni swa na Simba kulipa kisasi huku kila timu ikipata matokeo ya ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani.
mnyama SIMBA arudi kileleni mnyama SIMBA arudi kileleni Reviewed by Unknown on 02:35:00 Rating: 5

No comments

Recent