Home Top Ad

Responsive Ads Here

Watu zaidi wakamatwa kufuatia kifo cha Kim Jong-nam

Washukiwa wawili zaidi wamekamatwa kuhusiana na kifo cha Kim Jong-nam, ambaye ni ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un nchini Malaysia.
Mshukiwa mmoja mwanamke raia wa Indonesia na mwanamume raia wa Malaysia ambaye anakisiwa kuwa mpenzi wake wote walikamatwa leo Alhamisi.
Mwanamke mmoja maabye alikuwa na hati ya kusafiri ya Vietnam naye amekamatwa.
Kim alifariki siku ya Jumatatau kutokana na kile kinachaoimiw akuwa aliwekeka simu wakati akisubiri kuabiri ndeg mjini Kuala Lumpur.
Polisi wanasema kuwa wamemaliza kuufanyia uchunguzi mwili wake Kim licha ya matokeo kutotangazwa
Washukiwa hao wawili wa wamezuiwa rumande kwa siku saba.
Kuna uvumi unaoenea kuwa Korea Kaskazini ilihusika na mauaji hao.
Picha moja kutoka kwa kamera za usalama ambayo imepepeshwa nchini Korea Kusini na Malaysia, inaonyesha mwanamke mwenye fulana nyeupe yenye jina "LOL".
Inaaminiwa kuwa Kim alishambuliwa kwenye ukumbi wa kuabiri ndege kwenye uwanja wa ndege na wanawake wawili waliotumia aina fulani ya kemikali
Leo Alhamisi Korea Kaskazini inasherehekea kile kinachotajwa kuwa miaka 75 ya kuzaliwa kwa Kim Jong-il, mareheu kiongozi wa zamani na baba wa Kim Jong-nam na Kim Jong-un.
Watu zaidi wakamatwa kufuatia kifo cha Kim Jong-nam Watu zaidi wakamatwa kufuatia kifo cha Kim Jong-nam Reviewed by Unknown on 05:25:00 Rating: 5

No comments

Recent