Home Top Ad

Responsive Ads Here

Korea Kaskazini yafyatua kombora upande wa Japan

Korea Kaskazini kwa mara nyingine tena imefyatua kombora na kulielekeza upande wa pwani ya Japan.
Maafisa wa kijeshi kutoka Korea kusini wamekadiria kombora hilo limesafiri umbali wa kama kilo mita 500 hivi.
Serikali ya Korea kusini sasa imeitisha kikao cha kiusalama mjini Seoul .
Maafisa wa Pentagon nchini Marekani nao wamesema wamelifuatilia tukio hilo na kuongeza kuwa wamebaini ni kombora la masafa ya kadri.
Waziri wa mambo ya nje wa Korea kusini amesema vitendo kama hivyo vya uchokozi unaoendelezwa na Korea Kazkazini vinaonyesha dhahiri jinsi utawala jirani yao huyo usivyo na makini huku wakipania kuwa na zana za Nuclear.
Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe ambaye angali ziarani Marekani, ameshtumu ufyatuaji huo wa Kombora huku naye Rais Trump amemhakikishia Abe kuwa anamuunga mkono asilimia 100.
Harakati hizo za ufyatuaji wa kombora zinajiri siku moja tu baada ya mazungumzo kati ya rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe mjini Washington, ambako wamekubaliana kulipa kipa umbele swala la jinsi ya kukabiliana na vitisho vya zana za kinuklia kutoka Korea Kazkazini..
Korea Kaskazini yafyatua kombora upande wa Japan Korea Kaskazini yafyatua kombora upande wa Japan Reviewed by Unknown on 03:04:00 Rating: 5

No comments

Recent