Home Top Ad

Responsive Ads Here

KANUNI ZA UJASIRIAMALI

fuata kanuni zifuatazo kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kupitia ujasiriamali. 


1. Kuthubutu
Hii ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, hapa tunazungumzia uwezo na utayari wa kufanya maamuzi magumu ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara, mradi n.k. 
Wengi wanaogopa hasara, kuanguka mtaji au kufilisika. Mjasiriamali bora ni lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya mambo makubwa lakini uthubutu huo uendane na utafiti wa kina. Usiwekeze sehemu ambayo hujafanya utafiti wa kutosha.

2. Nidhamu
Hii pia ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali. Nidhamu ni muhimu sana katika biashara, matumizi ya pesa, muda, nidhamu kwa wateja na kila kitu kinachohusu shughuli zako zinazokuingizia kipato. Nidhamu ni chanzo cha mafanikio kwani ndiyo inayosimamia sehemu kubwa ya biashara zako.

3. Umakini

Wale waliofanikiwa sio tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi walizokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa makini kwa kila jambo, anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe na uelewa wa kutambua mabadiliko yanayojitokeza katika soko, uzalishaji na uendeshaji kwa jumla.

4. Uwezo wa kusimamia 
Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kuongoza na kusimamia biashara yake na kutoa uamuzi sahihi mara zote. Katika ujasiriamali, uwezo wa kusimamia na kuwaongoza watu wa chini yako ni muhimu sana kwani hata kama ukianza na biashara ndogo, lazima baadaye itakuwa kubwa hivyo utalazimika kuajiri watu wengine wa kukusaidia. 
Endapo utakosa uwezo wa kuwasimamia, ni dhahiri kwamba watakuibia, watafanya kazi tofauti na ulivyotegemea na mwisho utaanguka kibiashara.

5. Kujituma bila kusukumwa
Ili ufanikiwe katika biashara yoyote, lazima uwe na moyo wa kujituma na uipende kazi unayoifanya. Usisubiri kusukumwa kwa sababu hakuna atakayefanya kazi hiyo. Jifunze kuwahi kuamka asubuhi ili uendane na kasi ya soko, jitume kufanya mambo ambayo yataiboresha biashara yako bila kuchoka na fanya kazi kwa moyo wako wote.

6. Uaminifu
Uaminifu ni silaha kubwa itakayokulinda mjasiriamali na kuwafanya watu wengi wapende kufanya biashara na wewe. Jifunze kulipa madeni hata kama ni madogo unapodaiwa, wauzie wateja wako huduma au bidhaa kwa bei halali, lipia kodi na vibali vyote muhimu. Kamwe usiwauzie watu bidhaa zilizokwisha muda wake, zenye ubora hafifu au mbovu kwani kwa kufanya hivyo, wateja watakukimbia na huo ndiyo utakuwa mwisho wa biashara yako.


KANUNI ZA UJASIRIAMALI KANUNI ZA UJASIRIAMALI Reviewed by Unknown on 02:11:00 Rating: 5

No comments

Recent