Home Top Ad

Responsive Ads Here

Mshukiwa wa mauaji ya Kim Jong-nam alilipwa $90


Mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90, kushiriki katika kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.
Wanabalozi wa Indonesia waliokutana na Siti Aisyah, wanasema aliwaambia kuwa wanaume wawili, walionekana kama Wakorea au Wajapani, walimpa mafuta yaliofanana na yale ya mtoto kumpaka usoni mwanamme mmoja.
Mafuta hayo sasa yanafikiriwa yalikuwa na kemikali VX, moja kati ya sumu kali kabisa
Maafisa wa polisi wa Malaysia wanasema wataanza kufagia uwanja huo wa ndege ambapo shambulio hilo lilifanyika siku 12 zilizopita ili kuchunguza sumu yoyote iliosalia.
Maafisa wa polisi wa Malaysia walivamia nyumba yake huko Kuala Lumpur mapema wiki hii ili kuchunguza mauaji hayo.
Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo ,huku washukiwa wengine saba waisakwa na polisi ikiwemo raia wanne na Korea Kaskazini
Mshukiwa wa mauaji ya Kim Jong-nam alilipwa $90 Mshukiwa wa mauaji ya Kim Jong-nam alilipwa $90 Reviewed by pongwa trading on 21:29:00 Rating: 5

No comments

Recent