Mchezaji wa zamani wa Arsenal amesajiliwa Sweden, ni timu moja na Thomas Ulimwengu
Kiungo wa zamani wa Arsenal Emmanuel Frimpong amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden ambayo ni klabu anayocheza mtanzania Thomas Ulimwengu.
Klabu hiyo imepanda kucheza ligi kuu msimu huu ikitokea ligi daraja la kwanza imemsaini Frimpong siku chache baada ya nyota huyo mwenye miaka 25 kuvunja mkataba na klabu yake ya zamani Arsenal Tulaya Russia baada ya makubaliano ya pande mbili.
Frimpong alikuwa kwenye radar za Eskilstuna licha ya kutocheza kwa muda mrefu wakati akiwa Russia.
Eskilstuna wanataka kukiimarisha kikosi chao ili kufanya vyema kwenye mechi zao za ligi na wanaamini kwa kumsaini mchezaji huyo wa zamani wa Premier League kutasaidia kukipa nguvu kikosi chao na kumaliza katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.
Frimpong alisainiwa na Tula msimu uliopita sambamba na beki mwingine raia wa mwenzake wa Ghana Awal Mohammed lakini alicheza mechi tatu tu za ligi katika klabu hiyo.
Tangu alipoondoka Arsenal mwaka 2014, nahodha huyo wa zamani wa England U16 alicheza kwa mkopo Fulham Barnsley, Charlton pamoja na Wolverhampton Wanderers.
Mzaliwa huyo wa Kumasi- Ghana, alikulia kwenye academy ya Arsenal lakini hakupata nafasi ya kucheza kwa muda wa kutosha kwenye kikosi cha Arsenal chini ya Arsene Wenger.
Alibadili uraia kwa ajili ya kuitumikia timu ya taifa ya Ghana lakini kutokana na kiwango chake cha kupanda na kushuka akapoteza nafasi kwenye kikosi. Aliitwa mara mbili tu kwenye timu ya taifa ya Ghana.
Mchezaji wa zamani wa Arsenal amesajiliwa Sweden, ni timu moja na Thomas Ulimwengu
Reviewed by pongwa trading
on
01:48:00
Rating:
No comments