Home Top Ad

Responsive Ads Here

Kisa cha Man Fongo kumpandishia Msaga Sumu

Msanii wa muziki wa singeli Bongo, Man Fongo amemjia juu msanii mwenzake wa muziki huo, Msaga Sumu na kuikosoa kauli yake ya kujiita 'Mfalme wa Kisingeli' kwamba siyo kweli, na kwamba Msaga Sumu hana sifa za kujiita 'mfalme wa singeli'



Msaga Sumu abainisha kuwa wasanii wengi wa singeli hawana ubunifu, na ndiyo sababu muziki huo unaelekea kuwa kwa kuwa wanashindwa kutoa kazi zenye utofauti, huku akijiita kuwa yeye ndiye mfalme wa singeli Tanzania.
Man Fongo amesema "Kama anasema kwamba sisi hatuna uwezo siyo kweli na kama kweli yeye ni mfalme mbona hajaachia nyimbo tangu mwaka huu uanze? Mimi nitaachia nyimbo tuone kama haita sikika. Namuona Msaga Sumu kwangu bado kabisa kwa kuwa tunaimba aina tofauti ya muziki"
Hii ni ishara kuwa huenda Man Fongo akawa anakerwa zaidi na Msaga Sumu kujiita Mfalme wa Singeli
Hata hivyo Man Fongo amewasihi wasanii wa nyimbo za singeli kupendana ili kuweza kufanya mapinduzi makubwa katika muziki na kuweza kwenda sawa na muziki wa bongo fleva
Kisa cha Man Fongo kumpandishia Msaga Sumu Kisa cha Man Fongo kumpandishia Msaga Sumu Reviewed by Unknown on 03:11:00 Rating: 5

No comments

Recent