Home Top Ad

Responsive Ads Here

Aunty Ezekiel hakumbuki idadi ya mimba alizotoa

Msanii wa filamu nchi Tanzania Aunty Ezekiel amekiri kuwa katika maisha yake amewahi kutoa mimba na hakumbuki idadi ya mimba ambazo amewahi kuzitoa, huku akifichua siri kuwa amewahi kwenda kwa waganga kwa ajili ya kazi zake za sanaa.
Aunty amefunguka hayo leo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka LIVE kupitia ukurasa wa Facebook ambapo wananchi, wapenzi na mashabiki hupata fursa ya kuuliza mtu maswali na yeye hujubu mubashara.
Akijibu swali la shabiki wake mmojawapo aliyetaka kujua idadi ya mimba ambazo amewahi kutoa, Aunty amesema hawezi kusema uongo kuwa hajawahi kutoa mimba, lakini kitu ambacho hakumbuki ni idadi ya mimba alizowahi kutoa. "Kutoa nishawahi, nikisema sijawahi nitakuwa muongo, ila kukumbuka ni mimba ngapi ndiyo tatizo"
Aunty ambaye kwa sasa ana mtoto aliyezaa na dansa wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo, amesema kwa sasa anatamani zaidi kupata mtoto wa kiume atakamuita jina la Greyson ambalo ni jina la babu yake.
Msanii huyo pia ametaja idadi ya wanaume ambao amewahi kutoka nao kimapenzi huku akikanusha kutoka na marehemu Kanumba pamoja na Diamond Platnumz. "Hadi sasa nimeshatoka na wanaume kama sita au saba hivi"
Kwenda kwa waganga...
Lingine ambalo Aunty ameliibua leo ni kukiri kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa shida mbalimbali, ambapo baadhi ya mashabiki walitaka kujua kama na yeye ni mchawi, lakini akakanusha na kusema kuwa hajawahi kuwa mchawi ila amewahi kwenda kwa waganga kwa ajili ya shida zake mbalimbali ikiwemo masuala yake ya movie
"Mimi siyo mchawi, lakini kama ni kwenda kwa waganga huwa ninaenda nikiwa na shida zangu....... Ni kweli nimewahi kwenda kwa waganga kwa ajili ya kazi zangu za movie"

Alivyokutana na Mose......
Akisimulia jinsi alivyokutana na mpenzi wake wa sasa, Aunty amesema kuwa walikutana kwenye ndege wakiwa safarini kwenda Afrika Kusini na wakajikuta wakipendana.
"Mimi na Mose tulikutana na kupendana kwenye ndege tukiwa tunaenda Afrika Kusini, lakini tuliishia ku-kiss tu, tena mara moja, halafu mengine ndiyo yakaja kuendelea huku"
Akifafanua sababu za kumpenda Mose, Amesema "Mose ni mtu asiyeongea sana, akiwa kwa watu siyo mtu wa kuongea ovyo, lakini siyo kwamba haongei, ila anapokuwa kwa watu haongei, ni mpole na mtulivu. Napenda mwanaume ambaye siyo mropokaji"
Kuhusu umri wake Aunty amesema kwa sasa ana miaka 29 anaelekea wa 30 na ni mkubwa kuliko mpenzi wake. "Mimi ni mkubwa kwa Mose, ninamzidi umri sina hakika sana umri wake, nadhani ana miaka 26 sikumbuki vizuri lakini akili zake ni zaidi ya umri wake" Amesema Aunty huku akiweka wazi kuwa anatamani kumzalia watoto watatu". 
Kuhusu kupanga kuzaa na Mose, Aunty amesema kuwa ni kweli hakuwahi kupanga kuzaa na Mose, lakini ilitokea tu kama bahati, alipokutana naye akapata ujauzito, na yeye akaamua kumueleza Mose ukweli, na Mose akakubali ujauzito, na ndiyo maana hadi leo wako pamoja.
Asili ya jina lake......
Pia ameelezea chanzo cha yeye kuitwa Aunty, kuwa ni kutokana na shangazi zake kuwa wengi hala kila mmoja kugombea kumpa jina lake "Baba alivyonisimulia alisema wao walizaliwa 10, na yeye alikuwa wa kiume pekee, kwahiyo kila shangazi akataka nipewe jina lake, mwisho wa siku akaamua aniite shangazi ili kuwaridhisha wote"
Amesema jina lake la ubatizo anaitwa Gwantwa lenye asili ya Mbeya
Elimu yake....
Kuhusu elimu yake amesema aliishia kidato cha nne huku akipata Division Four na hana mpango wa kuendelea na elimu kwa kuwa anaamini kuwa hana akili za kusoma.
Aunty Ezekiel hakumbuki idadi ya mimba alizotoa Aunty Ezekiel hakumbuki idadi ya mimba alizotoa Reviewed by pongwa trading on 03:17:00 Rating: 5

No comments

Recent