Home Top Ad

Responsive Ads Here

Unene wahusishwa na aina 11 za saratani

Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kwamba wamethibitisha kuwepo kwa uhusiano mkubwa kati ya kunenepa na aina kumi na moja za saratani.
Watafiti wamebaini kwamba unene unasababisha saratani kadhaa ikiwemo saratani ya tumbo, ini, matiti, utumbo na nyumba ya mtoto.
Watafiti hao kutoka chuo kikuu cha Imperial mjini London, wanasema, kando na kuepuka uvutaji sigara, kutunza uzani unaozingatia afya bora, ndio njia moja muhimu inayopunguza uwezekano wa kuugua saratani.
Shirika la afya duniani linasema asilimia 40 ya watu wazima kote duniani ni wanene.
Unene wahusishwa na aina 11 za saratani Unene wahusishwa na aina 11 za saratani Reviewed by Unknown on 02:36:00 Rating: 5

No comments

Recent