Treni za umeme zinaletwa TZ, Dar-Moro? Dar- Dom? Dar-Mwanza
Hatimae serikali ya Tanzania kupitia
Wizara ya uchukuzi imesaini mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa Reli
ya kisasa itakayowezesha Treni zinazotumia umeme kuanza kufanya kazi
kwa mara ya kwanza Tanzania.
Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema ‘Sasa
hivi kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza unatumia saa 36 ambapo kuna
kilometa 1219 lakini Treni mpya za umeme zikianza kufanya kazi safari
itakua rahisi zaidi‘
‘Leo tunashuhudia utiaji saini
makubaliano ya ujenzi wa sehemu ya kipande cha reli kati ya Dar es
salaam na Morogoro chenye urefu wa kilometa 300 na mkataba huu utakua baina ya RAHACO kampuni hodhi ya rasilimali za reli na ubia kati ya kampuni ya UTURUKI na URENO’
‘Itakua
kwa gharama ya USD BILIONI 1, Milioni 215, laki 2 na 82 ikijumuisha VAT
USD Milioni 185 na laki 3, hii ni kwa ajili ya gharama za ujenzi kutoka
Dar es salaam mpaka Morogoro‘
‘Katika Afrika Treni kubwa
ambayo itakwenda spidi kubwa itakua ni ya Tanzania (Kilomita 160 kwa
saa), Treni nyingine itayokua na spidi kubwa itakua ni Morocco itakua
kilometa 200 kwa saa, naamini na sisi Tanzania tutabadilisha mawazo
kwenye Treni ya Dar Mwanza tutakua Kilometa 200 kwa saa‘
Kama hufahamu, wakati wa
utawala wa Uingereza marekebisho kidogo yalifanyika kwenye usafiri wa
Treni Tanzania kutoka Treni inayotumia mvuke kuja kwenye injini ya
Diesel, hata hivyo miundombinu hii kwa sasa ni chakavu na mwendokasi sio
chini ya Kilomita 30 kwa saa ambayo kutoka Dar kwenda Mwanza unachukua
saa 36‘ – Profesa Mbarawa
‘Mda wa mradi huu wa Umeme
kukamilika ni miaka miwili na nusu baada ya ujenzi kuanza, kutoka Dar es
salaam kwenda Morogoro Treni mpya ya umeme itatumia saa moja na dakika
16, Dar es salaam kwenda Dodoma itakua masaa mawili na nusu, Dar-Mwanza
saa saba na nusu’ – Profesa Mbarawa
Treni za umeme zinaletwa TZ, Dar-Moro? Dar- Dom? Dar-Mwanza
Reviewed by Unknown
on
23:35:00
Rating:
No comments